Gideon apongeza ushirikiano unaoendelea kushuhudiwa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa Chama cha, ODM Raila Odinga

Kwa mara nyingine Seneta wa Baringo, Gideo Moi amezungumzia siasa za mwaka 2022 akisema kuwa wakati huu ni wa kuwahudumia wananchi wala si kujihusisha na siasa za uchaguzi ambao bado haujawadia.  Moi aliyasema hayo katika mahojiano na Runinga na KTN.

Akizungumzia mabadiliko ya Katiba, Moi amesema Wakenya wana haki kisheria kufanya mabadiliko  kwani yatachangia vita dhidi ya ufisadi. 

Aidha  amepongeza ushirikiano unaoendelea kushuhudiwa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa Chama cha, ODM Raila Odinga akisema hatua hiyo imeleta utangamano miongoni mwa Wakenya.

Aidha ameyataja kuwa propaganda madai kwamba baadhi ya viongozi waliolenga kumtembelea babaye, ambaye ni Rais Mstaafu, Daniel Arap Moi walizuiwa kufanya hivyo. Moi amesema ziara hizo hazikuwa za kisiasa. Ikumbukwe Naibu wa Rais, William Ruto ni miongoni mwa waliokosa kumwona rais huyo mstaafu alipokwenda kumtembelea. Hata hivyo wengine waliofaulu kukutana naye ni Kinara wa Chama cha ODM, Raila Odinga, Kiongozi wa Chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka vilevile Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho.

Related Topics