Ndege aina ya Boeing 787-8 ya Shirika la Ndege la Kenya Airways iliyozinduliwa rasmi kwa safari za moja kwa moja kutoka uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kuelekea Marekani, inatarajiwa kutua katika Jiji la New York saa saba na dakika ishirini na tano adhuhuri saa za Kenya , ikiwa ni sawa na saa kumi na mbili na dakika ishirini na tano asubuhi saa za marekani.
Ndege hiyo ya moja kwa moja imerahisisha usafiri kwa kupunguza saa saba ambazo zilikuwa zikitumiwa kuunganisha ndege katika mataifa ya Uropa au Mashariki ya Kati. Kabla uzindunzi huo, safari ya kilomita 11,849 kutoka Kenya hadi Marekani ilichukua saa ishirini na mbili.