Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji amethibitisha kupokea faili kumi za ripoti ya uchunguzi kuhusu sakata katika taasisi ya Huduma za Vijana kwa Taifa NYS. Noordin amesema amepokea barua kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi DCI George Kinoti kumwarifu kuhusu ripoti hizo za uchunguzi. Aidha amesema kwa sasa kundi maalum katika ofisi yake litazithatimini faili hizo kabla ya kutoa mwelekeo zaidi kuhusu hatua zitakazochukuliwa.
Wakati uo huo, amewahakikishia wakenya kwamba ofisi yake inafanya kila iwezalo kulikabili tatizo hilo, huku akisema jopo kazi maalum lililoteuliwa kuendesha uchunguzi huo, limefanya kazi nzuri kufikia sasa.