×
App Icon
The Standard e-Paper
Home To Bold Columnists
★★★★ - on Play Store
Download Now

Safari za moja kwa moja kutoka Kenya-Marekani kuanza karibuni

Beatrice Maganga
Safari za moja kwa moja kutoka Kenya-Marekani kuanza karibuni
Shirika la Ndege la Kenya Airways, KQ siku ya Ijumaa linatarajiwa kuanza mpango wa kuwaruhusu wateja wake kulipia nafasi za usafiri wa moja kwa moja kutoka Kenya hadi jijini  Newyork Marekani. Kuanzishwa kwa safari hizo kutapunguza muda wa usafiri kutoka Kenya hadi Newyork kwa hadi saa 15 kutoka saa 22. KQ hata hivyo itatangaza baadaye siku kamili ambayo ndege ya kwanza itaanza safari zake.
Hayo yanajiri huku mawaziri watatu wakifanya ziara ya ghafla katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta, JKIA ili kukagua matayarisho ya uwanja huo  kwa safari hizo za moja kwa moja hadi Marekani.
Waziri wa Uchukuzi, James Macharia, Fred Matiang’i wa Masuala ya Ndani ya Nchi na mwenzake wa Utalii, Najib Balala walifika katika uwanja huo na kutangaza kuwa serikali imeteua kamati ambayo itawahusisha maafisa kutoka wizara hizo tatu na ambayo itashughulikia masuala ya safari hizo za ndege katika kipindi cha siku 100 zijazo.
Waziri Matiang'i amewataka maafisa katika uwanja huo kuwajibikia suala la usalama na kuwahudumia wasafiri kwa wakati ili kuepusha misongamano. Aidha ameagiza kukaguliwa kwa wahudumu wa texi wanaowasafirisha abiria baada ya baadhi yao kulaumiwa kwa madai ya kuwahangaisha wasafiri kwa kuwatoza ada za juu zaidi.
Waziri Balala aidha amesema Chuo cha Kitalii kitawapa mafunzo maafisa wote wa umma wanaofanya JKIA ili kuinua huduma katika uwanja huo.
..........
Get Full Access for Ksh299/Week
Unlock the Full Story — Join Thousands of Informed Kenyans Today
  • Unlimited access to all premium content
  • Uninterrupted ad-free browsing experience
  • Mobile-optimized reading experience
  • Weekly Newsletters
  • MPesa, Airtel Money and Cards accepted
Already a subscriber? Log in

Related Topics