Serikali yatangaza Novemba 28 kuwa likizo

Na, Suleiman Yeri
 
Serikali yatangaza  Novemba 28 kuwa likizo
 
Serikali kupitia Waziri wa Usalama wa Ndani ya Nchi, Fred Matiangi, imetanga Jumanne wiki ijayo kuwa likizo, kwa ajili ya hafla ya kuapishwa kwa Rais Mteule Uhuru Kenyatta.
Uhuru ataapishwa rasmi siku hiyo ambayo ni Oktoba tarehe 28 mwezi huu katika uwanja wa Kasarani kuhudumu kwa muhula wake wa pili na wa mwisho.
Maandalizi ya hafla hiyo yaendelea katika uwanja huo huku serikali ikutuma barua za mialiko kwa viongozi mbali akiwamo Aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama na Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
Inaarifiwa kuwa Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni tayari imetuma barua hizo kwa viongozi wote wa mataifa ya bara Afrika huku asilimia kubwa ya walioalikwa wakitarajiwa kuwasili nchini Jumatatu wiki ijayo.

Related Topics