Huna mamlaka yakurekebisha Matokeo Mahakama yamjibu ChebukatiHuna mamlaka yakurekebisha Matokeo Mahakama yamjibu Chebukati

Huna mamlaka yakurekebisha Matokeo Mahakama yamjibu Chebukati
by yeri
Mahakama ya Juu imedumisha uamuzi wa Mahakama ya Rufaa wa kumzuia ma Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, IEBC Wafula Chebukati kukarabati matokeo ya uchaguzi kutoka maeneo bunge na kusisitiza kuwa matokeo hayo kuwa ya mwisho na iwapo kuna dosari, zirekebishwe makamanani.
Akisoma uamuzi wa wengi wa majaji, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu amesisitiza kuwa jukumu la Chebukati ni kukagua fomu zote na kutangaza dosari zitakazogunduliwa kwa washikadau wote.
Hata hivyo atalazimika kuyatanga matokeo hayo jinsi yalivyo kabla ya kuwasilisha kesi katika mahakama ya uchaguzi.
Wakati uo huo Mwilu amesisitiza kuwa Chebukati ana jukumu la kukagua fomu zote zinazowasilishwa katika kituo cha kitaifa cha kukusanyia matokeo ili kuhakikisha kuwa hakuna dosari zozote.
Amesema jukumu la kukagua fomu hizo ni kuhakikisha uhalali wa uchaguzi na kuzia udanganyifu wakati wa shughuli wa ujumlishaji wa matokeo.
Wakati uo huo, Jaji Jackton Ojwang ameshikilia kauli iyo hiyo kwamba dosari za uchaguzi zinaweza tu kunakiliwa na upande ulio na malalamishi kushauriwa kuelekea mahakamani kutumia ushahidi ulionakiliwa.
Jaji Ojwang hata hivyo ametofautiana na wenzake na kusisitiza umuhimu wa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kukagua fomu zote ili kubainisha athari za dosari kwa matokeo ya uchaguzi kumwezesha mlalamishi kuamua iwapo ataelekea mahakamani au la.
Aidha licha ya kutoa ufafanuzi huo, Mwilu amesema mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kusikiliza ombi hilo. Hata hivyo wamechukua hatua ya kuisikiliza kwa manufaa ya umma

Related Topics