Matiang'i awataka polisi kuzingatia maadili ya utendakazi wakati wa uchaguzi

Na, Beatrice Maganga
Matiang'i awataka polisi kuzingatia maadili ya utendakazi wakati wa uchaguzi
Kaimu Waziri wa Masuala ya Ndani ya nchi, Fred Matiang'i ameelezea imani kwamba maafisa wa usalama watatekeleza jukumu lao kwa uadilifu wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Akihutubu wakati wa mkutano baina yake na wakuu wa usalama wa vitengo mbalimbali, Matiang'i ameonya kwamba huenda kukawa na visa vya kujaribu kuwachokoza maafisa wa usalama na kuwataka wazingatie sheria katika utendakazi wao.
Matiang'i amesema fotauti na ilivyodaiwa kwamba huenda maafisa wa usalama wnehtumiwa kuhujumu uchaguzi mkuu uliyopita, maafisa hao walizingatia maadili ya utendakazi na kufanikisha uchaguzi mkuu huru na wa haki.
Inspekta Mkuu wa Polisi, Joseph Boinett amerejelea kaunli ya Matiang'i kwamba polisi hawatakuwa na ubaguzi katika kuwahudumia wananchi wakati huu wa marudio ya uchaguzi.

Related Topics