Adah Ehi kupiga show ya kuombea Kenya Amani

Adah Ehi kupiga show ya kuombea Kenya Amani

Ada Ehi ni msanii maarufu Nigeria lakini pia ni msanii wa kimataifa wa gospel ambaye ametengeneza jina lake kwa muda sasa.

Mkali huyo mwenye kipaji cha aina yake ametua nchini Kenya kwa ajili ya kuombea Kenya amani wakati huu wa uchaguzi. Jumapili ya tarehe 30, July 2017, atakuwa Live kwenye tamasha moja kubwa kwa jina ‘Tukuza Festival’ ili kuhubiri amani Kenya.

‘Have just landed Kenya yesterday for the big Tukuza Festival to preache peace in Kenya. Its election time so we need to unit and fight against the spirit of evilness’ asema Ada.

Kupitia kipindi cha Konnect kinachoruka kila siku ya wiki pamoja na Clemmo 254 na Mwende, msanii huyo wa vibao kama ‘Only You Jesus‘ amefunguka wazi kuhusu tamasha hilo litakalofanyika kwenye ukumbi wa Arboretum Nairobi kwani nazo siku za uchaguzi zimesogea.

Hata hivyo, Ada ametaja wasanii wa Kenya anaowafahamu kama vile, Kambua, Size 8Reborn pamoja na Ringtone. Vile vile amependa wimbo wake Willy Paul, ‘Digirii’ na huenda akamtafuta na kufanya collabo naye.

Na,MkazivaeUNIT

Related Topics