Please enable JavaScript to view advertisements.
×
App Icon
The Standard e-Paper
Stay Informed, Even Offline
★★★★ - on Play Store
Download App

Walimu watano wakamatwa wakitoa mafunzo ya ziada

Na Beatrice Maganga

Polisi jijini Nairobi wanawazuilia walimu watano waliokamatwa wakiendeleza mafunzo ya ziada kwa wanafunzi katika Kanisa la House of Grace eneo la Lang'ata. Watano hao wamekamatwa kufuatia taarifa zilizotolewa kwa polisi na wananchi. Katibu katika Wizara ya Elimu Belio Kipsang aliwatuma maafisa wake walioandamana na maafisa wa polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Uwanja wa Nyayo kuongoza oparesheni ya kuwakamata.
Ilibainika kwamba wanafunzi zaidi ya hamsini kutoka shule mbalimbali walikuwa katika kanisa hilo wakifunzwa. Ilimlazimu Afisa anayehusika na viwango bora vya elimu John Okiya kuwaagiza wanafunzi hao kuelekea nyumbani.
Wiki iliyopita polisi vilevile waliivamia shule ya HappyLand Praparatory  iliyo mtaa wa Buruburu na kuifunga kwa kuendeleza mafunzo wakati wa likizo. Waziri wa Elimu Fred Matiang'i amesisitiza kwamba walimu watakaopatikana wakiendeleza mafunzo hayo watachukuliwa hatua.

Premium Article

Get Full Access for Ksh299/Week.

Bold Reporting Takes Time, Courage and Investment. Stand With Us.
Continue Reading  →
What you get
  • Unlimited access to all premium content
  • Ad-free browsing experience
  • Mobile-optimised reading
  • Weekly newsletters & digests
Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payments Kenya's most trusted newsroom since 1902
Support Independent Journalism

Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.

Journalism can't be free because the truth demands investment. At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate, factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the pursuit of credible journalism.

Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payment Kenya's most trusted newsroom since 1902