Marekani yaongoza kwa kujinyakulia medali huko Rio Brazil

 

Na,Hassan Ali

Ni siku ya sita mashindano ya olimpiki huko Rio Brazil na kila sekunde inavyofutika ndivyo jedwali la medali linavyobadilika. Marekani ingali kuongoza kukutu jedwali la medali kwa kujizolea jumla ya medali ya 26, dhahabu 9, fedha 8 na shaba 9. Nafasi ya pili inashikiliwa kwa sasa na Uchina iliyokwisha kujizolea medali 17, dhahabu 8 fedha 3 na shaba 6. Ukurasa wa tatu bora wafungwa na Hungary iliyokwisha kujinyakulia medali 6, dhahabu 4, fedha 4 na shaba 4. Barani Afrika kiongozi kwa sasa ni Afrika Kusini katika nafasi ya 25 ikiwa na medali 2 pekee za fedha. Kwa sasa Wakenya wanasubiri vijana wa raga kutinga uwanjani mnamo saa kumi na mbili jioni dhidi ya Japan, wakiwa na machungu kufuatia vipigo viwili vitakatifu kutoka kwa Great Britain na Newzeland.