Vijana wa James Nandwa wanapepetana na vijana wa Bandari

Na,Hassan Ali

Sasa hivi mechi mbili za ligi ya soka nchini zinaendelea  katika miji ya Thika na Nakuru. Mjini Nakuru uwanjani Afraha sasa hivi nyasi zaumia ambapo mwenyeji Ulinzi Fc baada ya kulitwaa taji la vikosi vya majeshi Afrika Mashariki inapambana na Posta Rangers waliowafunga Sofapaka bao moja kavu mnamo Jumapili iliyopita. Mjini Thika vijana wa James Nandwa wanapepetana na vijana wa Bandari ambao wamejitupa ugani wakiwa na mori kufuatia ushindi wao wa taji la KECOSO mjini Nakuru wikiendi iliyopita.