×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Wapenzi wa lugha-Tuzo za Kumikumi zilinoga

News
 Mwalimu-mtafiti-mwandishi-malenga-nguli, maarufu na mahiri Wallah bin Wallah Picha: Hisani

Mwalimu-mtafiti-mwandishi-malenga-nguli, maarufu na mahiri Wallah bin Wallah, kaandika saaana. Kafunza kwiingi! Na wasemavyo cha jasho hakikosi utamu.

Katokwa jasho kwapani akikimbizana na Kiswahilli, leo hii yeye sio kwamba tu anachangia mno makuzi na maenezi ya lugha ya Kiswahili kupitia vitabu na vyombo vya habari, lakini pia kwake nyumbani, Wasta Villa, eneo la Matassia (Ngong) viungani mwa jiji la Nairobi.

Mwalimu huyu mtajika kajenga ukumbi na maktaba ya wasomi, walimu, wanafunzi wa lugha kwenda kusoma, kufanya utafiti na kuhoji kuhusu Kiswahili. Ili kuwafikia wapenzi wa lugha walioko nje ya mipaka ya Kenya, kituo hicho cha Kiswahili, kikaasisi hafla maalum, sherehe mzo, tuzo ziitwazo Kumikumi.

Kila mwaka, tarehe kumi mwezi wa kumi shajara na kalenda ya Waswahili kote ulimwenguni kuna asteriski ya kumi kumi. Lengo na madhumuni kuwatuza ‘wangali hai’ wanahabari, walimu, waandishi, wanafunzi na wapenzi wote wa lugha ashirafu ya Kiswahili. Huo ulikuwa mwaka 2010, mwezi Oktoba tarehe kumi.

Ndio usuli na asili ya utatu wa kumikumi. Mwaka huu, kunako tarehe kumi mwezi Oktoba, ziliandaliwa tuzo hizo za kumikumi makala ya saba. Na zilinoga kweli. Zilifaulu hadi! Kama mwaka jana, makala ya mwaka huu yalivutia idadi kubwa ya wapenzi wa Kiswahili na ukumbi ulijaa pomoni.

Ulitapika! Usisahau sherehe za mwaka huu zilifanyika siku ya jumatatu. Wapo walionyimwa udhuru wakavunja miko ya kwahali kwao kwa kazi! Walii huvunja kanuni ati!

Mwalimu Wallah bin Wallah na mwanahabari mkongwe aliyewahi kufanya kazi na mashirika ya DW, BBC na sasa ni mhariri wa habari za michezo shirika la AZAM, Charles Hillary Martin, waliwaasa wanahabari kufanya tahadhari sana wawapo hewani hasa matumizi ya lugha.

Profesa Malonga alipopanda jukwaani kuelezea ni kwa vipi Kiswahili kinavyokua na kuzagaa nchini kwao Rwanda na nchi nyinginezo za ukanda huu kama Burundi, Uganda, Sudan Kusini na kwingineko, sote ukumbini tulipandwa na jazba. Madadi hasa!

Hafla ya mwaka huu ilitumiwa pia kuzindua vitabu viwili. MASHATENI WAMERUDI (Prof. S.A Mohammed) na VIFARU WEUSI (Dk. M.S. Khatib). 

Kwenye sherehe za mwaka huu vyombo vya habari pia vilipongezwa na kutuzwa kuokana na mchango wao katika kukuza lugha ya Kiswahili likiwemo jarida la Nairobian.

Hassan Ali ni Mhariri wa Michezo na Nahodha wa Nuruyalugha (RADIO MAISHA). [email protected], [email protected], FB: Ali Hassan Kauleni, Hassan mwana wa Ali, Twitter: @alikauleni

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles