Msamaha wa Rais

Na Mike Nyagwoka

Rais Uhuru Kenyatta ametia saini stakabadhi za kugeuza hukumu zote za vifo kuwa hukumu za maisha. Baada ya hatua hiyo katika ikulu, takriban wafungwa 2747 sasa wameponea kunyongwa. Rais ametumia kipengee cha 133 kwenye katiba kinachompa mamlaka ya kuwasamehe na kuwapunguzia vifungo wafungwa katika magereza nchini.
Mwanasheria Mkuu wa serikali Professa Githu Muigai, Waziri wa Masuala ya Ndani, Joseph Nkaissery, Kamishna wa Magereza, Isaiah Osugo, Mkuu wa Utumishi wa Umma, Joseph Kinyua na mwenyekiti wa Kamati ya Msahama wa Rais, Michael Kagika wamehudhuria hafla hiyo.