Please enable JavaScript to view advertisements.
×
App Icon
The Standard e-Paper
Smart Minds Choose Us
★★★★ - on Play Store
Download App

Kivumbi cha uongozi chaendelea kutifuka Nairobi

Na, Suleiman Yeri

Kinyang'anyiro cha ugavana Kaunti ya Nairobi kinazidi kuchacha huku Mbunge wa Dagoreti Kusini David Waweru, Mbunge Maalum Johnson Sakaja na Seneta Mike Sonko wakitangaza kubuni muungano wa kisiasa kwa jina, Team Nairobi.
Akizungumza baada ya kuhudhuria misa ya wafu katika eneo la Dagoreti, Sakaja amesema wameafikia uamuzi ambapo mmoja wao atateuliwa kuwania ugavana na mwingine naibu gavana kwenye Kaunti ya Nairobi, huku mmoja wao akiwania useneta.
Waweru amerejelea kauli yake kwamba wakazi wa Nairobi hawawezi kukubali kupendekezewa kiongozi na kuwasuta wanaotafuta uungwaji mkono kutoka kwa baadhi ya wabunge wa jiji hili.
Aidha wamesema ushirikiano baina yao unalenga kuwaletea maendeleo wakazi wa Nairobi na kuhakikisha wanashinda kiti hicho kwenye mchujo wa vyama na wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
Haya yanajiri siku chache baada ya Waziri wa Maji, Eugene Wamalwa kutangaza kushirikiana na Askofu Margaret Wanjiru kwenye kinyang'anyiro hicho.

Premium Article

Get Full Access for Ksh299/Week.

Bold Reporting Takes Time, Courage and Investment. Stand With Us.
Continue Reading  →
What you get
  • Unlimited access to all premium content
  • Ad-free browsing experience
  • Mobile-optimised reading
  • Weekly newsletters & digests
Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payments Kenya's most trusted newsroom since 1902
Support Independent Journalism

Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.

Journalism can't be free because the truth demands investment. At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate, factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the pursuit of credible journalism.

Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payment Kenya's most trusted newsroom since 1902