Wakenya waomboleza kifo cha Isaiah Kiplagat

Na,Hassan Ali

Wakenya wanaomboleza kifo cha aliyekuwa rais wa chama cha riadha nchini Isaiah Kiplagat. Kiplagat ameondoka duniani akiwa anatumikia marufuku kutoka kwa Shirikisho la Riadha Duniani, IAAF, yeye na wenzake David Okeyo na Joseph Kinyua,  kwa madai ya ufisadi.  Kiplagat alijiunga na chama  cha riadha nchini AK mwaka 1975 akiwa naibu wake mwenyekiti Charles Mukora, na kisha kutwaa uenyekiti wa AK mwaka 1992. Kiplagat aliyezaliwa Nandi huko Bonde la Ufa, alikuwa pia mwanachama wa IAAF tangu mwaka 1999. Aliwahi kukumbwa na maandamano ya wale waliopinga uongozi wake wakitaka ang’atuke mamlakani naye akawajibu
http://goo.gl/FeQ6Z1

Hivi marehemu katuachia nini nyuma?
http://goo.gl/iMdxPN
Aliwahi pia kuwania wadhfa wa naibu rais wa Shirikisho la Riadha Duniani.
http://goo.gl/1H0Scb
Na hii ndio kama iliyokuwa kauli yake ya mwisho kwa Wakenya
http://goo.gl/sUJxKF
Kwaheri ndugu Kiplagat na ulale salama