×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Moha Jicho Pevu: Ukiritimba Hague unaudhi

News

Wabunge wa Kenya hawaishi vihoja. Licha ya kutajwa kama bunge fisadi zaidi kuwepo - ukiongozwa na Spika asiyejali maslahi ya Wakenya - wabunge hawa wetu sasa wamepeleka uozo wao katika mahakama ya jinai huko Hague, Uholanzi.

Wengi watakubaliana nami kwamba taifa letu laongozwa na baadhi ya viongozi waliokosa maono, yani ni wajinga kupindukia.

Nasikitika kuwaona wasomi wetu wananapojifanya kutoelewa tofauti baina ya usiku na mchana.

Badala ya kutunga sheria za kuwafaidi wakenya, wao wameamua kutunga sheria za kumkomboa mtu mmoja na sio wakenya milioni 44.

Bila shaka Uholanzi imeshangazwa na tabia za kitoto za wabunge zetu, wabunge wasio na hekima wala utaifa.

Bila haya wameridhia kuvuja mamilioni ya pesa, pesa za walipa ushuru kuzuru Hague na kuonyesha ukiritimba wao mbele ya macho ya dunia. Dunia nzima sasa wanafahamu fika kuwa wabunge wetu hulipwa kufanya upuzi na vihoja kote kote.

Kwa pamoja wabunge hawa mamluki wamefilisi taifa hili na kuhakikisha maskini atazidi kuwa maskini huku tajiri akizidi kuwa tajiri.

Kamwe wamesahau kuwakilisha kina mama na watoto waliochomwa ndani ya kanisa la kiambaa. Pia wamewasahau wakenya waliouawa huko Eldoret, Naivasha na maeneo mengine yalioathirika na ghasia za baada ya uchaguzi.

Mabwenyenye hawa wamekuwa kama mungu wa maskini. Kwa miaka 52 tangu uhuru wetu, kiwanda cha mkenya wa kawaida kimekuw ni kile cha jua kali- kiwanda cha huzalisha watumwa wakuwafanyia kazi matajiri fisadi.

Lakushangaza ni kwamba wakenya tumeshindwa kukabiliana na genge hili licha ya nguvu na sauti moja tuliyonayo.

Genge hili la kabila ndogo la ufisadi kamwe haifai heshima. Mbona tuwaheshimu huku wao wamekosea waajiri wao wapiga kura heshima sampuli hii?

Naomba waseme sala zao za mwisho kwani maskini ameerevuka. Ifikapo mwaka wa 2017, tutawabwaga nje bila woga. Ni wakati huu ambapo watoto wa maskini watajitosa ugani kupigania nafasi za kuwakomboa maskini wenzao kutoka kwa minyororo ya utumwa.

Njooni tushirikiane ili tuepuke maovu haya. Kwa pamoja muwachague vijana chapa kazi, wenye sifa kede kede na rekodi safi. Kamwe msiangalie kabila, dini wala utajiri wao. Angalieni utajiri wa moyo.

Kwa sasa serikali hii inabeba mimba ya mamba, mimba itakayokuwa chungu kuzaa mwaka wa 2017, mwaka wa kuwanyoa na mabati iliyo na kutu. Waacheni wachezee mali yenu, haki zenu na kubaka katiba kwa kipindi cha miaka mitano maana sioni wakibadilika. Lakini msisahau kuwaadhibu ipasavyo siku hiyo ya kupiga kura.

Msiwasaze hawa majangili hata kwa sekunde moja. Msisahau walivyowafanya mafukara, msisahau walivyonunua mipira ya kondomu, msisahau walivyonunua kalamu na sabuni kwa bei za kipumbavu, msisahau walivyonunua wheel barrow kwa fikra za kishenzi, msisahau walivyofuja pesa zenu.

Ni wazi kuwa wabunge wetu wanaabudu miungu binadamu, hata hawastahili kuitwa waheshimiwa! Wafagilieni waovu wote mwaka wa 2017.

Mohammed Ali ni Mhariri Mkuu wa Kitengo cha Upekuzi KTN. Kuwasiliana naye: [email protected], FB: Official Jicho Pevu with Mohammed Ali, Twitter: @mohajichopevu

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles