KNHRC, UDM on senate

Hisia mbali mbali zinaendelea kutolewa kuhusiana na pendekezo la kuondolea mbali bumnge la seneti. Pendekezo hilo lililotolewa na mbunge wa ndaragwa jeremiah kioni, limepingwa vikali. Wabunge 10 wanaoegemea chama cha UDM, wamesema waasisi wa pendekezo hilo ni maadui wakubwa wa suala la ugatuzi na kwamba wanapania kujinufaisha kisiasa. Tume ya utetezi wa haki za kibinadamu khrc mkurugenzi wake atsango chesoni, imesema amesema wazo la kioni halina msingi wowote kwa kuwa serikali ya senate ndiyo inayoweza kuendeleza ugatuzi na usamabazi wa hela na raslimali huko mashinani.