Kenya Sudan Diplomatic row Kisw

Mzozo wa kidiplomasia kati ya kenya na sudan unatokota. Leo khartoum imempa balozi wa kenya nchini humo saa 72 kuondoka nchini humo, na kumuita nyumbani balozi wake mara moja. Khartoum imeghadhabishwa na agizo la jana la mahakama kuu kuwa bashir anayesakwa na mahakama ya icc, akikanyaga humu nchini atiwe nguvuni. Khartoum bungeni mbunge wa kirinyaga Joseph Gitari ameitaka wizara ya mambo ya nje kuwahakikishia wakenya wanaoishi sudan kuwa wako salama kufuatia mzozo huu. Kenya amekuwa mshirika mkuu wa sudan tangu kutoa mchango mkuu kupatikana kwa ule mkataba wa amani kati ya kusini na kaskazini, na hatimaye sudan kusini kuwa taifa huru.