Kongowea market filth

Wafanyibiashara katika soko la Marikiti mjini Mombasa wamefanya mgomo mapema hii leo na kususia kuendelea kuuza bidhaa zao kutokana na kile walichokitaja kama mazingira machafu ndani ya soko hilo. Wafanyi biashara wa soko hilo wamelilaumu baraza la jiji la mombasa kwa kuzembea katika uzoaji taka na hivi basi kuchangia kwa kulundikana kwa takataka nje ya soko hilo linalouza vyakula mbalimbali na hivi basi kuzua hofu ya mkurupuko wa maradhi.