Bishops on national schools

Kanisa katoliki leo limeiomba serikali kuwahusisha katika mpango wa kuzipandisha hadhi shule za upili za mikoa hadi za kitaifa. Hatua hii inajiri baada ya pendekezo la kutaka kuongeza idadi ya shule za kitaifa kutoka 18 hadi 105. Tume ya elimu ndani ya kanisa hilo chini ya uenyekiti wa askofu Maurice Crowley imesema kati ya shule 87 zinazolengwa kupandishwa hadhi, ishirini ziko chini ya uongozi wa kanisa katoliki na huzingatia pakubwa maslahi ya wanafunzi kutoka jamii maskini na kusema kuwa wanahofia kuwa wanafunzi hao huenda wakakosa nafasi iwapo shule hizo zitafanywa za kitaifa