KCSE celebrations [Swa]

Kuna msemo usemao kila mtu huvuna anachopanda, na hatimaye matunda ya mavuno hayo yameonekana huku wanafunzi wakijitokeza kusheherekea matokeo ya mtihani wa kidato cha nne KCSE. Shule ya wavulana ya Alliance ilidhihirisha ubabe wake kwa kutwaa nafasi ya kwanza kitaifa na vilevile kutoa mwanafunzi wa pili kitaifa Marube Machuka Allan. Shule ya upili ya Moi Kabarak ndiyo iliyotoa mwanafunzi aliyeongoza nchini, Wandua Albert Kamau. Kenya High nayo ikatoa msichana aliyeongoza kitaifa Lydia Katini Mwangasha. Ili kukujuza kuhusu jinsi washindi walivyosheherekea mwanahabari lulu hassan amekuwa akifuatilia kwa karibu mbwembwe hizo na kutuandalia taarifa ifuatayo….