Transport: Mwakwere speaks out

Sekta ya uchukuzi imekumbwa na changamoto sio haba; sio migomo ya matatu ,  mpangilio duni wa uchukuzi katikati mwa jiji na pia wasiwasi mwingi uliozingira usafiri wa ferry katika kivukio cha Likoni. Matatizo haya yote sio ya leo ni matatizo ambayo yamekuweko miaka nenda miaka rudi na kidole cha lawama kimeonekana kuelekezwa pande tofauti kwa idara ya trafiki, kwa wizara ya uchukuzi na waziri wake Chirau Mwakwere hajaepuka. Kwenye mahojiano ya kipekee na KTN Leo jioni hii mwanahabari Anne Ngugi alipata fursa kumdadisi Mwakwere kuhusu lalama hizo na ukweli wa mambo kwa mtazamo wa waziri Mwakwere.