Serikali imebuni kamati maalum itakayochunguza madai ya kuwapo kwa sumu kupita kiasi ya aflatoxins kwenye bidhaa hasa za mahindi nchini. Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri na Mwenzake wa Biashara Peter Munya wamesema kwamba wamebuni kamati hiyo ambayo inawahusisha wataalam mbalimbali kuchunguza suala hilo.
Munya amesema kwmaba Wizara yake inaendelea kufuatilia suala hilo ili kuhakikisha kwamba vyakula vinavyouzwa nchini vinaafikia viwango vinavyokubaliwa kwa matumizi ya binadamu.