Mavazi yanayomweka kiongozi wa kike kwenye mizani

Wanawake na mavazi. Je unapomuona mwanamke ama msichana yeyote, jambo la kwanza ambalo huwa waangalia ni nini? Ni mavazi au ni nywele ama ni vipodozi? Na iwapo huyu mwanamke anataka kuwa kiongozi kwa mfano, utamhukumu na nini ukimwona kwa mara ya kwanza? Mavazi? Ni majeli yake (maumbile) ama utangoja azungumze? Kwa kweli sisi wanadamu tunao uzoefu wa kuwahukumu wenzetu kwa maumbile yao ya nje tu kabla ya jambo jingine lolote.

Ukipatana na mtu yeyote utamwangalia na kum? kiria kwa namna fulani kulingana na vile alivyovaa. Basi jambo hili linawaathiri wanawake kwa sana kuwaliko wanaume. Leo acha tuongee kuhusu mavazi hasa ya wanawake na wasichana uongozini. Je mavazi yana umuhimu upi katika mwanamke anayetaka kuwa kiongozi, sharti avae nguo fulani? sharti awe na nywele fulani na uso wake kupakwa mafuta kwa jinsi fulani? Hili ni swali nililowauliza vijana wenzangu tulipokuwa tunapiga gumzo pale mtaani.

Ra? ki yangu mmoja kwa jina Adera alikuwa na maono haya:  “Mimi nadhani kuwa mwanamke aliye katika uongozi ama anayetaka kuchaguliwa sharti avae nguo rasmi wakati wowote, zenye heshima na zinazomwonyesha kuwa ni kiongozi. Ninapom? kiria kiongozi, namuona mwanamke mwenye masuti meusi na nywele nzuri zisizo na madoido. Namuona na marinda na masketi yaliyoshonwa kwa ustadi, ili akiweza kusimama pale kwenye jukwaa kuongea, hata kabla hajasema jambo, sote tunamuona kama kiongozi wetu.” Ananiambia Adera.

Ra? ki yangu wa pili kwa jina Halima alisema hivi: “Mimi nadhani haifai kuwa na ? kra fulani kuhusu mwonekano wa kiongozi mwanamke. Naona ni kama siyo vizuri kuwahukumu wanawake wanaogombea uongozi kwa mavazi wanayovaa. Hasa kama ni kina dada wenye umri mdogo kama sisi sidhani kama ni haki kutarajia wasichana wanaotaka kuwa viongozi kuanza kuvaa marinda na vitenge kama kina mama wengine ndio waridhishe jamii.

Ni Bora kila mtu avae na kuonekana anavyohisi yuko sawa vile, pasi na kulazimishwa kuonekana kwa namna fulani na jamii. Bora awe amefunika mwili, asivae nguo fupi sana na kutuonyesha mapaja , asibanwe na sketi sana na kuwakosesha vijana barubaru amani na kuwavunja shingo, mimi sina shida ya vazi la mwanamke katika uongozi. Nitamsikiza wala sitamhukumu kwa mwonekano wake ama alivyovaa.

Ni kweli kwamba wengi wetu tuko kama Adera. Mavazi ni umuhimu mno kwa mwanamke anayegom bea kiti cha uongozi. Akija bila vitenge na ‘weaves’ nono nono basi huyo hatoshi mboga. Lakini swali ni, je haya mavazi yanametusaidia kuwapata viongozi wazuri?

Labda ndio, labda la. Kwa upande mwingine, wanaume kama magavana Mike Sonko na Hassan Joho wameweza kuchaguliwa pasi na kuvaa masuti. Mike Sonko ameonekana mara nyingi akitembea na mavazi ya kawaida tu na mikufu yake ya dhahabu kwenye mikutano kadhaa. Hakuna aliyesema kuwa hawezi kumchagua kwa sababu ya mavazi yake.

Mimi binafsi sipendi suti, sipendi vitenge, nywele yangu sipendi kusuka bali napendelea tu mtindo wa ‘shagy  hair. ‘ Isitoshe, napenda sana kuvaa longi wala sipendi marinda na sketi. Na siku za usoni nina ndoto ya kuwakilisha jamii yangu bungeni. Sijui kama wataniambia niende nikavae marinda marefu, sijui kama watasema nikasongwe nywele ama nibandike ‘wigs’ kutoka Uhina? Sijui kama watasema  nivae vitenge? Sijui kama lipstick (rangi yam domo) yangu nyekundu itawakera?

Baadaye sijui kama itanibidi nifanye hayo yote, niwe mtu tofauti na mimi mwenyewe, ili kuwafurahisha wapiga kura, halafu nikichachaguliwa nirudie maisha ama mtindo wangu wa kawaida? Hiyo si ni kujidanyanya? Mimi sipendi kujidanganya na sipangi kuwadanganya, ndiposa naomba sana kuwa jamii yangu itanipokea kama nilivyo, itazisikiza sera zangu, na kunipa fursa bila ya kunilazimisha kuvaa vitenge virefu na nywele ya farasi, na kuendesha magari meusi ya kuazima.

Kwani kwa miaka mingi tumewachagua wenye huo mwenendo. Na shida ni zile zile. Vitenge na nywele za kubandikwa hazijatutatulia shida. Vuti vyeusi kwa kweli havijatujengea barabara. Basi ni vyema tuache viongozi wavalie watakavyo kwa raha yao.