Upatanishi au urafiki? Kibarua cha Tony Blair kukamilika Mashariki ya Kati

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair amesita kuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa Mashariki ya Kati. Kuangazia muda wake akiwa mjumbe, itabainika wazi kwamba hakufanikisha lolote katika mzozo huo. Wakosoaji wake wanasema amejiweka karibu sana na serikali ya Israel na hawezi kuwajibika kutetea masilahi ya Wapalestina.

Kwa upande mwingine, wadadisi wanaelewa kwamba jukumu la kazi yake Mashariki ya Kati ilikuwa pana mno. Hakuweza kudokeza viegezo madhubuti kupanua uhuru wa Wapalestina kusafiri mji wa Gaza na maeneo yaliyokaliwa na Israel. 

Ni dhahiri shahiri kwamba kazi ya wapatanishi Mashariki ya Kati ni ngumu sana. Wadau wengi katika siasa za eneo hili hawajaweza kufanikishwa kupata suluhu kwa changamoto zinazowakumba Wayahudi na Waarabu.

Mzozo huu unaendelea kuzua hali ya utata kwenye eneo la Mashariki ya Kati. Itabidi mataifa wafadhili wa mazungumzo ya amani kama Marekani, Ufaransa, Urusi, Uingereza na Ujerumani yashinikize pande zote mbili zinazozozana kufikia makubaliano. Hususan kuhusu  mji wa Jerusalem na pia suala la walowezi wa Kiyahudi katika eneo zilizokaliwa na Israel.

 

Professor David O. Monda

Dept. of Social Science

National University - California.