Unamlea vipi mwana wako? Bila shaka,ulezi ni njia mojawapo ya mzazi kumpa mwana maisha marefu,ili apate kuinuki na maadili mema katika jamii. Lakini kuna tofauti ipi kati ya ulezi wa kileo na ule wa miaka ya nyuma? Jee unaweza kumchapa mwanayo ambaye amekwenda kinyume na kanuni hasa zinazoongoza familia yako? Ali Manzu,analichambua swala la ulezi kando na kubaini ni kwa nini wazazi wengine hushindwa kuwalea watoto wao na kuwaachia serikali kuchukua udhibiti wa ulezi na kufunza tabia njema.