Profesa Wangari Muta Maathai, mshindi wa tuzo la amani la nobel mwaka wa 2004 amefariki. Wangari maathai aliyepata umaarufu wake kupitia juhudi zake za uanaharaki wa kulinda mazingira alifariki usiku wa kuamkia leo, katika hospitali ya nairobi, baada ya kuugua saratani ya mfuko wa mayai kwa muda. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa ban ki-moon ameomboleza kifo cha maathai aliyemtaja kama kielelezo chema katika utetezi wa haki. Wangari Maathai amefariki akiwa na umri wa miaka sabini na moja.