Wauguzi warejea kazini baada ya kuusitisha mgomo wao

News

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, Athari za mgomo wa Madaktari nchini zinatarajiwa kupunguwa kwa kiwango fulani, baada ya wauguzi kuusitisha mgomo wao Jumatano na kukubali kurejea kazini.

Mgomo wa wauguzi hao ulisitishwa jana alasiri baada ya wao kutia sahini makubaliano kati yao na serikali za kaunti 47 nchini ambazo zimekubali kuutambua muungano wao.

Aidha, Muungano huo chini ya Katibu Mkuu Seth Panyako umekubali nyongeza ya mishahara iliyotolewa na serikali Jumapili iliyopita.

Baadhi ya maafikiano hayo ni kuwa, wauguzi walio katika daraja la G hadi L watapata marupurupu ya shilingi elfu ishirini na walio katika daraja la M na zaidi, watapata marupurupu ya shilingi elfu kumi na tano kila mwezi.

Nyongeza hiyo itatolewa kwa awamu mbili ya asilimia 60 mwezi Januari mwaka ujao na asilimia 40 mwezi Julai.

Athletics
Were out to prove his dominance at Kip Keino Classic
Athletics
Eldoret City Marathon stars have gone ahead to rule global contests
Hockey
SCHOOL: Musingu and Tigoi Girls show their class in schools hockey
Athletics
Hellen Obiri leads Kenya's Boston Marathon sweep