Huduma za afya Kenyatta kutatizwa

News

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, Huduma za Afya katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta zinatarajiwa kutatizwa zaidi baada ya washauri waliokuwa wakihudumu hospitalini humo kusitisha huduma zao Jumatano jioni, na hivyo kuwaacha wauguzi na madaktari wa Jeshi la Kenya, KDF kuwahudumia wagonjwa.

Zaidi ya washauri 300 ambao ni wanachama wa Muungano wa Madktari, KMPDU wamesema kuwa wamekuwa wakitoa huduma zao tangu mgomo wa wahudumu wa afya kuanza japo serikali haijaonyesha ishara na nia ya kuyashughulikia matakwa yao.

Katibu Mkuu wa KMPDU, Ouma Oluga amesema washauri hao wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu ikizingatiwa uchache wa wauguzi.

Wakati uo huo, hospitali za binafsi katika Kaunti ya Kakamega zinaendelea kuripoti idadi kubwa ya wagonjwa, huku mgomo wa madaktari ukiendelea.

Kufikia jana, Hospitali ya Rufaa ya Kakamega ilikuwa imefungwa licha ya agizo la Muungano wa Wauguzi kuwataka wauguzi kuusitisha mgomo wao na kurejea kazini.

Inaarifiwa kuwa wagonjwa kutoka maeneo ya Lurambi, Butere, Mumias na viunga vyake wanaendelea kuwasili katika hospitali ya Kimishonari ya St. Marys Mumias ambako wasimamizi wamesema huenda wakalemewa na idadi kubwa ya wagonjwa.

Wadi ya akina mama wajawazito tayari imejaa.

By Jonah Onyango 49 mins ago
Volleyball and Handball
Chumba back as KCB aim to reclaim continental title in Cairo
By AFP 1 hr ago
Sports
Kenya's Munyao gets better of Bekele to win London Marathon
By AFP 7 hrs ago
Football
Arsenal thrash Chelsea 5-0 to open up Premier League lead
By AFP 7 hrs ago
Football
Inter Milan seal Scudetto in derby thriller with AC Milan