Serikali kuzishughulikia familia za polisi waliofariki Naivasha

News

Na Carren Omae

Serikali itashughulikia mahitaji ya familia za maafisa kumi na mmoja wa polisi waliofariki dunia katika ajali ya barabarani eneo la Naivasha Jumamosi usiku. Akizungumza alipoongoza ibada ya wafu kwa ajili ya maafisa hao katika Ikulu ya Nairobi, Rais Kenyatta amewapongeza maafisa hao kwa kujitolea katika kazi zao.

Kauli hiyo ya Rais imetiliwa mkazo na Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Jospeh Nkaiserry Kwa upande wake, Inspekta Mkuu wa Polisi, Joseph Boinett amesema taifa limewapoteza sio tu maafisa wa polisi bali pia watumishi wa umma waliojitolea katika kuyatekeleza majukumu yao, bila utepetevu wowote.

Maafisa hao ni miongoni mwa watu 43 waliofariki dunia katika ajali hiyo iliyotokea Jumamosi usiku. Hafla hiyo imehuduriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo mawaziri, wabunge na viongozi wa dini.

Volleyball and Handball
Chumba back as KCB aim to reclaim continental title in Cairo
By AFP 21 hrs ago
Sports
Kenya's Munyao gets better of Bekele to win London Marathon
By AFP 1 day ago
Football
Arsenal thrash Chelsea 5-0 to open up Premier League lead
By AFP 1 day ago
Football
Inter Milan seal Scudetto in derby thriller with AC Milan