Wauguzi wakubaliana na serikali kuhusu matakwa yao

News

Na Beatrice Maganga

Hatimaye Serikali, Chama cha Wauguzi, KNUN  na Baraza la Magavana zimetia saini makubaliano kuhusu matakwa ya wauguzi. Makubaliano hayo yameafikiwa baada ya mapema leo  wauguzi kuondoka katika mkutano wa kutafuta mwafaka.

Hata hivyo walirejea katika mkutano huo saa za adhuhuri.  Akizungumza wakati wa mkutano wa kutia saini makubaliano hayo, Waziri wa Afya Cleopa Mailu ametoa changamoto kwa madaktari kufuata mkondo huo wa wauguzi na kushiriki mazungumzo ili kupata suluhu.

Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Peter Munya vilevile amewataka madaktari kurudi kazini kufuatia agizo lililotolewa jana na Mahakama ya Uajiri na Leba kuwataka wasitishe mgomo. 

Football
FKF, Fifa launch women football campaign
Golf
All set for 'Hole in One' mega prize at Kambsome tourney Seafront Mombasa
Athletics
It has been 60-year dominance in athletics as other sports struggle
Football
Sevilla wins Europa League as Montiel clinches another penalty shootout