Na Mate Tongola
NAIROBI, KENYA, Aliyekuwa Makamu wa Rais nchini Sudan Kusini Riek Machar anaendelea kuzuiliwa nchini Afrika Kusini.
Inaarifiwa kuwa Machar ambaye alitorokea taifa la Congo mapema mwezi Agosti mwaka huu baada ya vita kuzuka kati ya walinzi wake na Rais Salva Kiir, anazuiliwa chini cha kifungu cha nyumbani.
Zaidi ya watu milioni moja wametoroka makwao katika taifa hilo changa zaidi ulimwenguni tangu ghasia kuzuka mwishoni mwa mwaka 2013 wakati Kiir wa jamii ya Dinka alipomfuta kazi Machar wa jamii ya Nuer.