Shinikizo la kumtaka Karua kujiunga na Jubilee zazidi

News

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, Wawakilishi sita wa Wadi katika Kaunti ya Kirinyaga wametishia kutounga mkono azma ya kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua ya kuwania ugavana eneo hilo iwapo hatajiunga na mrengo wa Jubilee.

Wakiongozwa na Kiongonzi wa Wengi katika bunege la Kaunti hiyo Kinyua Wangui, Wawakilishi hao wamesema Kirinyaga ni ngome ya Jubilee na hivyo sharti Karua ajiunge na chama hicho iwapo ana nia ya kutwaa wadhifa huo.

Wiki kadhaa zilizopita, Karua alitangaza msimamo wake kuhusu kutojiunga na Jubilee licha ya Rais Uhuru Kenyatta kutoa wito wa kujiunga nao, wakati wa ziara yake eneo hilo.

Athletics
Were out to prove his dominance at Kip Keino Classic
Athletics
Eldoret City Marathon stars have gone ahead to rule global contests
Hockey
SCHOOL: Musingu and Tigoi Girls show their class in schools hockey
Athletics
Hellen Obiri leads Kenya's Boston Marathon sweep