Serikali kuchunguza kilichosababisha ajali eneo la Naivasha

News

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, Wakenya wametakiwa kusalia watulivu huku serikali ikiendeleza uchunguzi wa mkasa wa juzi eneo la Naivasha ambapo watu arubaini waliaga dunia baada ya gari lililobeba kemikali kusababisha ajali.

Waziri wa Masuala ya Ndani mwa Taifa Joseph Nkaissery amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa gari hilo aina ya Canter lilikuwa likisafirisha kemikali hiyo kuelekea Uganda kabla ya kukosa mwelekeo karibu na soko la Kinungi, Naivasha na kuyagonga magari mengine 14.

Tayari miili ya waliofariki imesafirishwa hadi hifadhi ya maiti ya Chiromo, Nairobi huku shughuli ya kuitambua miili hiyo ikiwa imeshika kasi.

Miongoni mwa walioaga dunia na maafisa kumi na moja wa GSU ambao walikuwa wametoa huduma za ulinzi kwa Rais Uhuru Kenyatta ambaye alikuwa ziarani eneo la Bomet.

Naibu wa Rais William Ruto ni miongoni mwa waliotuma rambirambi kwa waliowapoteza wapendwa wao kwenye ajali hiyo.

Wakati uo huo, Rais Uhuru Kenyatta ameahirisha ziara yake katika kaunti ya Narok iliyotarajiwa kuanza Jumanne kufuatia ajali iliyotokea katika eneo la Karai kaunti ndogo ya Naivasha.

Katika ujumbe msemaji wa Ikulu Manoa Esipisu amesema rais atatumia mda huo kuzitembelea na kuzifariji familia za mafisa kumi na mmoja wa kikosi cha GSU kitengo cha kuwalinda watu maarufu ambao ni miongoni mwa watu 40 waliofariki dunia wakati wa ajali hiyo.

Athletics
Kenya hoping to defend World Cross Country title in Belgrade
Football
Fifa threatens Kenya with ban again
Unique Sports
SCHOOLS: Lenana School, Kisumu Girls and Agoro Sare turn focus on national games finals
Motorsport
Safari Rally: 29 drivers set for epic showdown as Safari Rally zooms off