Koome aitaka IEBC kuwahakikishia Wakenya uchaguzi huru Agisto tiasa

Jaji Mkuu Martha Koome ameitaka Tume ya Uchaguzi IEBC kushughulikia kwa haraka masuala makuu yaliyosababisha kubatilishwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017.

Akizungumza wakati wa kikao na Chama wa Wahariri Nchi kuhusu utayarifu wa Idara ya Mahakama kushughulikia kesi za baada ya uchaguzi, Koome amesema kuwa nyingi ya masuala hayo yalihusu utendakazi wa IEBC.

Koome amesema tume hiyo inastahili kuwaeleza Wakenya namna imeweka mikakati ya kuzuia kurudiwa kwa hali iliyoshuhudiwa hasa kuhusu kusambazwa na kutangazwa kwa matokeo ya kura za urais.

Kikao hicho pia kulijadili suala la wawaniaji wenye kesi mbalimbali mahakamani  hasa baada ya IEBC kusema kuwa hawawezi kuzuiwa hadi rufaa walizowasilishwa zitakaposilikizwa na kuamuliwa. Jaji Daniel Musinga anaeleza amesisitiza umuhimu wa hilo kuzingatiwa.

Koome amesema jumla ya kesi 168 za kura ya mchujo zinasikilizwa na Mahakama ya Kutatua Migogoro ya Vyama Kisiasa, 29 zikishughulikiwa na Mahakama Kuu na moja katika Mahakama ya Juu.

By Stephen Rutto 42 mins ago
Athletics
Kenyan stars ready for World Cross showdown in Belgrade
Motorsport
Safari Rally 2024: Tanak urges Kenyan children to take up motorsports as a career
Rugby
SCHOOLS: From the classroom to the field, Kisumu Girls ready to lift national rugby trophy
Motorsport
Safari Rally 2024: Neuville clinches Kasarani stage as Hyundai makes intention known