Nimetoa damu mara 32

General Podcasts | 1 month ago

Katika podcast yetu leo hii, tunazungumza na Joseph Maina ambaye ametambuliwa na serikali ya Kaunti ya Turkana hasa Wizara ya Afya kuwa bingwa wa kutoa damu kwa mara 32 tangu mwaka 2019. Maina ni fundi wa kutengeneza simu katika Mji wa Lodwar na husafiri mara nyingi kila sehemu ya nchi anapohitajika kutoa damu. Mwanahabari wetu wa Turkana, Mike Ekutan ametangamana naye kuzungumzia kwa kina kuhusu safari yake ya kujitolea kutoa damu.