Gumzo na Mwanaspoti Podcast: Nitawainua wachezaji - Twaha Mbarak, Sehemu ya 2

Gumzo na Mwanaspoti | 3 months ago

Wachezaji katika kaunti zote arubaini na saba nchini watanufaika na uongozi wa Twaha Mbarak iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka FKF. Katika sehemu ya pili ya mahojiano na Ali Hassan Kauleni, Mbarak anasema atawahusisha washikadau wote ili kuhakikisha kwamba wachezaji kutoka kaunti mbalimbali wanajumuishwa katika kikosi cha timu ya kitaifa ya soka Harambee Stars.