Kisa Changu Podcast: Sina mikono; mahangaiko na kusaidiwa -Jackline Mwende, Sehemu ya 2

Kisa Changu | 4 months ago

Katika sehemu ya kwanza ulifahamu kuhusu kilichofanya Jackline Mwende kupoteza mikono yote miwili. Katika sehemu hii ya pili, Mwende anaeleza namna ambavyo sasa inamlazimu kuwategemea watu wengine hasa wazazi wake kumfanyia majukumu hata ya kimsingi kama kumwosha. Aidha, anasema hali yake ya maisha imewasababishia mahangaiko makubwa wazazi wake na hata kuwasababishia matatizo ya kiafya. Maisha ya Mwende - mama wa mtoto mmoja yamebadilika vipi tangu tukio hilo la miaka 5 iliyopita? Sikiliza podcast hii.