Vijana na Mapenzi; inakera kwa mume kushauriwa na wazaziwe kabla ya kufanya lolote?

Vijana na Mapenzi | 1 week ago

Mwanamume anapokuwa mtu mzima, wengi hutarajia kwamba awe mwenye kujitegemea kimawazo na hata kuweza kujifanyia maamuzi ya busara. Hata hivyo, kuna wanaume ambao huitwa 'mamas boy' ambao hushtumiwa kwa kutojitegemea kimawazo na kuwasikiliza zaidi wazazi kabla ya kufanya maamuzi muhimu. Je, ni sawa kwa mume kuzingatia zaidi ushauri wa mzazi badala ya mkewe?