Uchumi na Biashara Podcast; Biashara ya maji imeninunulia ploti na nyumba

Uchumi na Biashara | 5 months ago

Maji ni uhai, ni hitaji la kila mtu. Hapa jijini Nairobi, kuna wakati watu hawana maji katika nyumba zao, na ndipo Justus Ambani sawa na wengine wengi, hujihusisha na kazi ya kuuza maji kutumia mkokoteni. Ambani anayeendesha shughuli hii katika mitaa ya Fedha na Tassia Embakasi Mashariki, anasema kupitia biashara hii amenunua kipande cha ardhi vilevile nyumba. Esther Kirong' amemhoji katika makala ya leo ambapo anasema aliacha kazi ya kuajiriwa kisha kujiajiri. Ameweza kuwaajiri wengine wakiwamo vijana.