SECTIONS

Katika siku za hivi maajuzi kumekuwa na ongezeko la visa vya wanaume kuwaua jamaa zao na wakati mwengine wao pia kujitia kitanzi au kutoroka baada ya kutekeleza maovu hayo. Lakini maswali yanayochipuka ni mbona mtu akawaua awapendao zaidi  badala ya kutatua matatizo yoyote ambayo huenda yanamuandama baina yake na jamaa zake?