Mamlaka ya Kutathmini Utendakazi wa Maafisa wa Polisi, IPOA imetilia mkazo juhudi za Rais William Ruto kuhakikisha kwamba maafisa wa polisi waliotumia vyeo vyao kuwadhulumu raia wanaadhibiwa.
Katika kikao na Wanahabari, Mwenyekiti wa IPOA Anne Makori ameapa kuhakikisha kwamba hakuna kisa cha polisi kumdhulumu mtu kinakosa kuchunguzwa na adhabu kutolewa.