Rais, Uhuru Kenyatta hatimaye amezindua rasmi matumizi ya barabara ya mwendo-kasi ya Nairobi Express Way baada ya ujenzi wake kukamilika.
Akizungumza wakati wa shughuli ya uzinduzi huo, Rais amesema kwamba chini ya uongozi wake Kenya imepiga hatua kubwa katika kuimarisha muundo msingi.