Premium

Sikuambii Unisaidie! Ruto amwambia Uhuru

Mgombea urais wa UDA, Naibu wa Rais William Ruto ameendeleza shutma dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta kwa kuisuta manifesto yake huku akimhusisha na mapungufu serikalini. Akiwahutubia wakazi wa Meru, Ruto amesisitiza kutengwa serikalini na kamwe Rais hafai kumlaumu. Aidha, amemtaka kujiondoa katika siasa za mwaka huu, akisema hashindani naye bali Raila Odinga.

Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung'wa kwa upande wake amemtaka Rais kuubeba msalaba wake bila kumlaumu Ruto.

Pia Ruto amefutilia mbali madai kwamba analenga kumfungulia mashtaka Rais Kenyatta iwapo atashinda urais. Anasema halengi kivyovyote kumwandama Rais bali mawakala wa kisiasa ambao wanatumia taasisi za umma kujitajirisha, matamshi ambayo yametiliwa mkazo na Kindiki.

Wakati uo huo, Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amepuuza kauli ya Rais kwamba Waziri wa Kilimo Peter Munya ameimarisha sekta ya kilimo. Kwa mujibu wa Nyoro, masaibu ya wakulima yameongezeka wakati wa uongozi wa Munya. Pia amemsuta kwa kupunguza bei ya unga kwa shilingi mbili.

Ruto amekuwa Mlima Kenya kwa siku ya pili leo hii, ili kujitafutia asilimia kubwa ya kura miongoni mwa wapigakura takribani milioni milioni tano waliosajiliwa na Tume ya Uchaguzi IEBC.

Related Topics

Rais, Ruto, Kenyatta