Huku idara ya Elimu kaunti ya Kilifi ikiripoti kuongezeka kwa viwango duni vya masomo miongoni mwa wanafunzi kaunti hiyo, baadhi ya viongozi wanakashifu hatua ya serikali kupiga marufuku sherehe za mazishi maarufu kama Disco Matanga inayotajwa kuchangia mimba za mapema na matokeo duni ya mitihani.
Mwakilishi wadi ya Mtepeni Kaunti ya Kilifi Victor Mwaganda Gogo ameeleza kuwa sherehe hizo zimesaidia pakubwa katika kumaliza umasikini sawa na kuwapa vijana ajira ili kukimu mahitaji yao.