Please enable JavaScript to view advertisements.
×
App Icon
The Standard e-Paper
Stay Informed, Even Offline
★★★★ - on Play Store
Download App

Jitihada za kukabili ukame zaendelea

Na, Sophia Chinyezi,

Shirika la Msalaba Mwekundu limetia saini mkataba wa makubaliano na Shirika la Kitaifa la Sekta za Binafsi KEPSA, ili kukabili ukame unaoshuhudiwa nchini. Akiongoza hafla hiyo mapema leo katika hoteli moja jijini Nairobi, Waziri wa Masuala ya Humu Nchini, Joseph Nkaissery amepongeza hatua hiyo, akisema kuna haja ya serikali ya Kitaifa na zile za kaunti kutenga fedha za kukabili majanga mbalimbali.
Nkaissery ametaja baadhi ya mikakati iliyowekwa na serikali kuwaepushia Wakenya athari za ukame, huku akizipa changamoto serikali za kaunti kuiga mfano wa juhudi hizo na kuanzisha hazina ya kukabili majanga. Aidha amesikitishwa na hatua ya kaunti kujitokeza wakati wa dharura badala ya kujiandaa mapema kukabili majanga endapo.
Kuhusu suala kwamba kila kaunti itatoa shilingi milioni moja kwa Shirika la Msalaba Mwekundu ili kukabili baa la njaa, Nkaissery amesema kiwango hicho ni cha chini mno, ikizingatiwa kuwa ukame umewaathiri zaidi ya watu milioni 1.3.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa shirika hilo, Abbas Gullet amesema kuna mpango wa kuchangisha shilingi bilioni moja ili kushughulikia janga hilo na kuongeza kuwa mikakati ya kusambaza fedha kwa waathiriwa hao imewekwa.

 

Premium Article

Get Full Access for Ksh299/Week.

Fact-first reporting that puts you at the heart of the newsroom. Subscribe for full access.
Continue Reading  →
What you get
  • Unlimited access to all premium content
  • Ad-free browsing experience
  • Mobile-optimised reading
  • Weekly newsletters & digests
Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payments Kenya's most trusted newsroom since 1902
Support Independent Journalism

Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.

Journalism can't be free because the truth demands investment. At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate, factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the pursuit of credible journalism.

Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payment Kenya's most trusted newsroom since 1902

Follow The Standard on Google News

Related Topics