Maandalizi yanaendelea kabla ya ziara ya siku mbili ya Rais William Ruto katika eneo la Nyanza.
Akizungumza na wanahabari katika Ikulu ya Rais ya Kisumu Msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed amesema kwamba ziara ya siku mbili katika eneo la Nyanza inalenga kutimiza baadhi ya ahadi alizotoa kwa wakazi wa eneo hilo hapo awali.
Hussein aidha amepuzilia mbali hofu kwamba hakuna fedha za kutosha za kugharamia miradi mbalimbali ya kimaendeleo akisema kuna mikakati maalum ya kufadhili miradi hiyo.