×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Wabunge waongoza maandamano Bungoma

News

Mbunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga  na mwenzake wa Webuye Mashariki Dan Wanyama wamewaongoza wakazi wa Chwele katika Kaunti ya Bungoma kufanya maandamano ya amani kulalamikia ongezeko la visa vya ajali kwenye maeneo bunge hayo.

Waandamanaji walifunga Barabara Kuu ya  Lwakhakha -  Chwele - Bokoli na kuzuia matrela yanayopita  kwenye barabara hiyo wakisema ni chanzo cha visa vya ajali hizo.Viongozi hao wanasema barabara hiyo ilitumika wakati wa janga la covid 19 ili kupunguza msongamano kwenye mpaka wa Malaba ila imeendelea kutumika baada ya msongamano huo kuisha.

Wamemtaka Waziri wa Barabara na Uchukuzi Kipchumba Murkomen kuingilia kati suala hilo.

Kwa upande wao wakazi wamelalamikia ajali nyingi ambazo zimesababisha vifo na ulemavu kwa waathiriwa wa ajali katika barabara hiyo wanayosema ni ndogo mno.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week