Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ameendelea kuwashauri wanasiasa wa eneo la Kati ya Nchi kuunga mkono serikali iliyopo kwa manufaa ya wakazi wa Mlima Kenya.
Akizungumza katika kaunti ya Nyeri alipoongoza halfa ya kufuzu kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mt. Kenya, Naibu huyo wa Rais, amesisitiza kwamba sasa msimu wa siasa umeisha na kwamba kuna haja ya viongozi wa matabaka mbalimbali kuungana.