×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Spika Wetangula atangaza viti vya Eneo Bunge la Garissa Mjini na Kandara kuwa Wazi

News

Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetangula  ametanagza kuwa wazi nyadhfa za ubunge katika Eneo Bunge la Kandara na Garissa Mjini.

Kupitia taarifa katika Gazeti Rasmi la Serikali Spika Wetnagula amesema hatua hiyo inafuatia uteuzi wa Alice Wahome na Adan Duale kuwa mawaziri.

Spika Wetangula amesema watu wana uhuru wa kufanya kampeni Tume ya Uchaguzi-IEBC ikitarajiwa kutangaza tarehe rasmi ya uchaguzi mdogo.Aden Duale aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na  Alice Wahome Waziri wa Maji, Usafi wa Mazingira na Unyunyiziaji Maji Mashamba.

Spika wa Seneti Amason Jefwa Kingi pia anatarajiwa kutangaza nafasi za Seneta Kipchumba Murkomen ambaye ni Waziri wa Uchukuzi kuwa wazi.

Aidha Chama cha UDA pia kitalazimika kumteua seneta mwingine maalum kuchukua nafasi ya Soipan Tuya ambaye sasa ni Waziri wa Mazingira

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week